Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika kikao na balozi wa nchi ya Iran, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini sanjari na kulaani kitendo cha jinai cha utawala wa Kizayuni cha kuishambulia Iran na kuuawa shahidi makamanda wa kijeshi na wananchi, alisisitiza msimamo wa serikali na wananchi wa nchi yake sambamba na serikali na Taifa la Iran katika kutimiza malengo yake matukufu na kutetea matakwa na haki halali za wananchi wa Iran.
Amesisitiza kuwa, Serikali na wananchi wa Afrika Kusini wanalaani vitendo vya kinyama vya utawala wa kibaguzi wa Israel dhidi ya wananchi wa eneo la kikanda hususan watu wa Palestina, Lebanon na Iran.
Your Comment